Watumwa

Watumwa wote wawahesabu mabwana zao kuwa wanastahili hesh ima zote, ili watu wasije wakalitukana jina la Mungu pamoja na mafundisho yetu. Watumwa ambao mabwana zao ni waamini, wasikose kuwaheshimu kwa kuwa ni ndugu; bali watumike kwa ubora zaidi kwa sababu wale wanaonufaika kwa huduma yao ni waamini na ni wapendwa.

Fundisha na kuhimiza mambo haya. Mtu ye yote akifundisha kinyume cha haya na asikubaliane na maneno ya kweli ya Bwana wetu Yesu Kristo, na mafundisho yanayo ambatana na kumcha Mungu, huyo amejaa majivuno na wala hafahamu cho chote. Mtu kama huyo ana uchu wa ubishi na mashindano ya maneno ambayo huleta wivu, ugomvi, matukano, shuku mbaya, na ugomvi wa mara kwa mara kati ya watu wenye mawazo maovu, ambao hawanayo ile kweli, na ambao hudhani kwamba kumcha Mungu ni njia ya kuchuma fedha.

Bali kumcha Mungu na kuridhika ni faida kubwa. Kwa maana hatukuja na kitu cho chote hapa duniani, wala hatuwezi kutoka na kitu. Lakini kama tuna chakula na mavazi, basi tutaridhika. Watu wanaotamani kuwa matajiri huanguka katika majaribu na mtego na katika tamaa nyingi mbaya na za kijinga, ambazo huwato komeza wanadamu katika upotevu na maangamizi. 10 Maana kupenda fedha ni chanzo cha uovu wote. Tamaa ya fedha imewafanya wengine watangetange mbali na imani na kuteseka kwa huzuni nyingi.

Mawaidha Ya Paulo Kwa Timotheo

11 Lakini wewe mtu wa Mungu, epuka haya yote. Tafuta kupata haki, utauwa, imani, upendo, subira na upole. 12 Pigana ile vita njema ya imani. Shikilia uzima wa milele ulioitiwa ulipokiri lile ungamo lako jema mbele ya mashahidi wengi.

13 Mbele ya Mungu ambaye amevipa vitu vyote uhai, na mbele ya Kristo Yesu ambaye kwa ushuhuda wake mbele ya Pontio Pilato alikiri lile ungamo jema, 14 ninakuamuru utunze amri hii bila doa wala lawama mpaka Bwana wetu Yesu Kristo atakapokuja. 15 Jambo hili Mungu atalitimiza kwa wakati wake mwenyewe, Mungu Mbarikiwa ambaye peke yake ndiye Atawalaye, Mfalme wa wafalme na Bwana wa mabwana. 16 Yeye peke yake ndiye asiyekufa, na ndiye aishiye katika nuru isiyoweza kukaribiwa; hakuna mwanadamu ali yepata kumwona wala awezaye kumwona. Heshima na uweza una yeye hata milele. Amina.

17 Uwaagize matajiri wa ulimwengu huu waache kujivuna, wala wasiweke matumaini yao katika mali ambayo haina hakika. Bali wam tumaini Mungu ambaye hutupatia vitu vyote kwa wingi ili tuvifu rahie. 18 Waambie watende wema, wawe matajiri katika matendo mema, wawe wakarimu na tayari kushiriki mali zao na wengine. 19 Kwa njia hii watajiwekea msingi imara kwa wakati ujao na hivyo watajipatia uzima ambao ni uzima kweli.

20 Timotheo, tunza vema yote uliyokabidhiwa. Epuka majadil iano yasiyo ya Mungu na mabishano ambayo kwa makosa huitwa elimu.