Timotheo Atumwa Kwenda Thesalonike

Hatimaye tuliposhindwa kuvumilia zaidi, tuliona afadhali tubaki Athene peke yetu. Tukamtuma Timotheo ambaye ni ndugu yetu na mtumishi wa Mungu katika kuieneza Habari Njema ya Kristo, aje kuwaimarisha na kuwatia moyo ili asije mtu akababaishwa na mateso haya. Kama mjuavyo, tumepangiwa mateso. Hata tulipokuwa pamoja nanyi tuliwaambia mara kwa mara kwamba tutateswa, na kama mjuavyo ndivyo ilivyokuwa. Ndio maana niliposhindwa kuvumilia nilituma mtu ili nifahamu msimamo wenu katika imani. Niliogopa kuwa pengine yule mjaribu shetani alikuwa amewajaribu na kwamba pengine juhudi yetu kwenu ingekuwa ni bure.

Taarifa Ya Timotheo

Lakini sasa Timotheo amekwisha rejea kutoka kwenu na ameleta taarifa nzuri kuhusu imani yenu na upendo wenu. Ametuam bia kwamba mnatukumbuka kwa wema na kwamba mna hamu siku zote kutuona kama nasi tulivyo na hamu ya kuwaona. Kwa sababu hiyo ndugu zetu, katika dhiki na mateso yetu yote tumefarijika kwa ajili yenu, kutokana na imani yenu. Maana sasa hakika tunaishi kwa kuwa ninyi mmesimama imara katika Bwana. Tutawezaje kumshu kuru Mungu kiasi cha kutosha kwa ajili yenu, kutokana na furaha tuliyo nayo mbele za Mungu wetu kwa sababu yenu? 10 Usiku na mchana tunaomba kwa bidii ili tuwezeshwe kuwaona tena na kuwapa tieni kile ambacho bado kinapungua katika imani yenu.

11 Tunamwomba Mungu, Baba yetu mwenyewe na Bwana wetu Yesu atutayarishie njia ya kuja kwenu. 12 Bwana na awawezeshe ninyi kupendana zaidi na zaidi na kuwapenda watu wote kama sisi tunav yowapenda ninyi. 13 Tunamwomba awaimarisheni mioyo ili msiwe na lawama bali muwe watakatifu mbele za Mungu Baba yetu, wakati Bwana wetu Yesu atakapokuja pamoja na watakatifu wake wote.