Kutoka kwa Paulo na Timotheo, watumwa wa Yesu Kristo. Kwa watakatifu walioko Filipi pamoja na maaskofu na wasaidizi wote wa kanisa. Tunawatakieni neema na amani itokayo kwa Mungu Baba yetu na kwa Bwana wetu Yesu Kristo. Shukrani Na Maombi.

Ninamshukuru Mungu wangu kila ninapowakumbuka katika sala zangu zote, nikiomba kwa furaha na shukrani kwa ajili ya ushi rikiano uliopo kati yetu katika kueneza Injili, tangu siku ya kwanza hadi leo. Nina hakika kwamba, yeye aliyeianza kazi yake njema mioyoni mwenu, ataiendeleza na kuikamilisha siku ile ataka porudi Yesu Kristo.

Ninajisikia hivi kwa sababu nawathamini sana moyoni mwangu. Kwa maana tumeshiriki pamoja neema ya Mungu wakati nikiwa kifun goni na wakati nikiitetea na kuithibitisha Injili. Mungu ni shahidi wangu kwamba natamani mno kuwa pamoja nanyi na kwamba upendo nilio nao kwenu ni upendo wa Kristo Yesu. Na sala yangu kwa ajili yenu ni kwamba upendo wenu uzidi kuongezeka siku hadi siku pamoja na maarifa na busara 10 ili mpate kutambua mambo yaliyo mema. Na pia mpate kuwa watu safi, wasio na hatia hadi siku ya Kristo. 11 Maisha yenu yawe na matunda ya haki yatokayo kwa Yesu Kristo, ili Mungu apewe utukufu na sifa. 12 Ndugu zangu, napenda mfahamu kwamba haya mambo yaliyonipata yamesaidia sana kueneza Injili ya Kristo. 13 Watu wote hapa pamoja na maaskari wa ikulu wanajua wazi kuwa mimi niko kifungoni kwa sababu ya kumtumikia Kristo. 14 Kwa sababu ya kifungo changu, ndugu wengi katika Bwana wametiwa moyo kuhubiri neno la Mungu pasipo hofu. 15 Ni kweli kwamba wapo ndugu wengine wanaom hubiri Kristo kutokana na wivu na kwa kutaka kushindana; lakini wengine wanamhubiri Kristo kwa nia njema. 16 Hawa wanahubiri kwa moyo wa upendo, wakifahamu kwamba Mungu ameniweka hapa kifungoni ili niitetee Injili. 17 Hao wengine wanamtangaza Kristo kwa tamaa ya kupata sifa wala si kwa moyo wa upendo, wakifikiri kwamba kwa kufanya hivyo wataniongezea mateso yangu kifungoni. 18 Lakini kwangu mimi hiyo si kitu. Lililo la muhimu ni kwamba kwa kila njia Kristo anahubiriwa, ikiwa kwa nia mbaya au kwa nia njema. Kwa sababu hiyo, mimi nashangilia. Pia nitaendelea kushan gilia, 19 kwa sababu najua kwamba kwa ajili ya sala zenu na kwa msaada wa Roho wa Yesu Kristo, jambo lililonipata litageuka kuwa njia ya kufunguliwa kwangu. 20 Shauku yangu na tumaini langu ni kwamba sitaaibika kwa njia yo yote, bali nitakuwa na ujasiri, ili kama ilivyo sasa, Kristo aendelee kutukuzwa kutokana na maisha yangu, kama ni kuishi au hata kama ni kufa. 21 Kwa maana kwangu mimi, kuishi ni Kristo na kufa ni faida. 22 Kama nitaendelea kuishi katika mwili, hii itaniwezesha kufanya kazi yenye matunda. Lakini sijui nichague lipi! 23 Yote mawili yananivutia: nata mani niyaache maisha haya ili nikakae pamoja na Kristo, jambo ambalo naona ni bora zaidi. 24 Lakini kwa sababu yenu naona kuwa ni muhimu zaidi nikiendelea kuishi. 25 Nina hakika kwamba, kwa sababu hii nitabaki na kuendelea kuishi pamoja nanyi nyote, ili mpate kukua na kuwa na furaha katika imani. 26 Na hivyo, kwa ajili yangu, muwe na sababu ya kuona fahari ndani ya Kristo Yesu kwa kuja kwangu kwenu.

Mapambano Kwa Ajili Ya Imani

27 Lakini hata ikitokea nini, hakikisheni kuwa mwenendo wenu unalingana na Injili ya Kristo. Ili kama nikija kuwaona au hata nisipojaliwa kufika, nipate habari kuwa mnasimama imara katika roho ya umoja, mkiwa na nia moja huku mkipambana kwa pamoja kwa ajili ya imani ya Injili, 28 bila kuwaogopa wale wanaowapinga. Hii ni ishara dhahiri ya kuangamia kwao, lakini kwenu ninyi, hii ni ishara ya wokovu wenu kutoka kwa Mungu. 29 Kwa maana mmepewa heshima kwa ajili ya Kristo, sio tu kumwamini, bali pia kuteswa kwa ajili yake. 30 Sasa mnashiriki mapambano yale yale mliyoona nikiwa nayo na ambayo mnasikia kwamba bado naendelea nayo.