Adhabu Ya Babiloni

17 Mmoja wa wale malaika saba waliokuwa na yale mabakuli saba akaja akaniambia, “Njoo, nitakuonyesha hukumu ya yule kahaba mkuu aliyeketi juu ya maji mengi. Wafalme wa dunia wamezini naye, na watu waishio duniani walilewa divai yake ya uzinzi.” Kisha nikiwa katika Roho malaika akanipeleka nyikani, nikamwona mwanamke mmoja ameketi juu ya mnyama mwekundu aliyejaa majina ya kumtukana Mungu mwili mzima. Mnyama huyo alikuwa na vichwa saba na pembe kumi. Huyo mwanamke alikuwa amevaa mavazi ya rangi ya zambarau na nyekundu na kujipamba kwa dhahabu, vito vya thamani na lulu. Mkononi mwake alishika kikombe cha dhahabu kilichojaa mambo ya kuchukiza na uchafu wa uasherati wake. Na kwenye kipaji cha uso wake yaliandikwa maneno yenye maana iliyofichika: “Babiloni Mkuu, Mama wa Makahaba na wa Machukizo yote ya Duniani.”

Read full chapter