Mnyama Kutoka Ardhini

11 Kisha nikamwona mnyama mwingine akipanda juu kutoka katika ardhi. Alikuwa na pembe mbili kama za mwana kondoo lakini aliongea kama joka. 12 Naye alitumia uwezo wote wa yule mnyama wa kwanza aliyemtangulia. Akalazimisha dunia yote na wote waliomo duniani wamwabudu huyo mnyama wa kwanza aliyekuwa na jeraha la kifo lililokuwa limepona. 13 Huyu mnyama wa pili akafanya miu jiza ya ajabu hata kufanya moto utoke mbinguni na kushuka duniani mbele ya watu. 14 Kwa njia ya miujiza aliyowezeshwa kufanya kwa niaba ya yule mnyama wa kwanza, aliwadanganya watu waishio duniani. Aliwaamuru watengeneze sanamu kwa heshima ya yule mnyama aliyekuwa amejeruhiwa kwa upanga lakini akaishi. 15 Kisha akawe zeshwa kuipatia pumzi ile sanamu ya mnyama wa kwanza hata ikaweza kuongea na kufanya wale wote ambao hawakuiabudu wauawe. 16 Pia aliwalazimisha watu wote, wakubwa kwa wadogo, matajiri na mas kini, watu huru na watumwa, watiwe alama kwenye mikono yao ya kulia au kwenye vipaji vya nyuso zao. 17 Hakuna mtu ye yote ambaye angeweza kununua au kuuza kitu kama hana alama ile, yaani jina la huyo mnyama au namba ya jina lake.

18 Jambo hili linahitaji hekima. Mwenye akili ya kutambua apige hesabu ya mnyama huyo kwa sababu ni namba ya mtu. Namba yake ni mia sita sitini na sita.

Read full chapter