46 Mnamo saa tisa Yesu akalia kwa sauti kuu, “Eli, Eli lama sabakthani?” Yaani, “Mungu wangu, Mungu wangu, mbona ume niacha?”

47 Baadhi ya watu waliokuwa wamesimama hapo waliposikia haya walisema, “Anamwita Eliya!” 48 Mmoja wao akaenda mbio akaleta sponji akaichovya kwenye siki akaiinua kwa mwanzi akamwekea mdo moni. 49 Lakini wengine wakasema, “Hebu tuone kama Eliya ata kuja kumwokoa.” [Na mwingine akachukua mkuki akamchoma ubavuni, pakatoka maji na damu].

50 Yesu akalia tena kwa sauti kuu, kisha akakata roho.

Read full chapter