15 “Mtakapoona lile ‘Chukizo la Uharibifu’ linalozungumzwa na nabii Danieli limesimama mahali Patakatifu - msomaji na aelewe - 16 basi wale walioko Yudea wakimbilie milimani. 17 Aliyeko juu ya nyumba asishuke kuchukua vitu vyake ndani. 18 Aliyeko sham bani asirudi nyumbani kuchukua vazi lake. 19 Ole wao wanawake watakaokuwa na mimba na watakaokuwa wakinyonyesha siku hizo! 20 Ombeni ili mtakapokuwa mnakimbia, isiwe ni kipindi cha baridi au siku ya sabato. 21 Kwa maana kutakuwa na dhiki kuu ambayo haijawahi kutokea tangu mwanzo wa dunia mpaka sasa na ambayo haitatokea tena. 22 Kama siku hizo zisingepunguzwa, hakuna hata mtu mmoja ambaye angesalimika, lakini kwa ajili ya wale walioteu liwa na Mungu, siku hizo zitapunguzwa. 23 Wakati huo mtu aki waambia, ‘Tazama! Kristo yuko hapa!’ au ‘Kristo yule pale!’ msi sadiki. 24 Kwa maana watatokea makristo na manabii wa uongo na watafanya ishara za ajabu na miujiza mingi ili kuwadanganya, hata ikiwezekana, wateule wa Mungu. 25 Angalieni, nawatahadharisha mapema.

26 “Kwa hiyo wakiwaambia, ‘Yule kule nyikani,’ msitoke. Au wakisema, ‘Yuko chumbani 27 Kwa maana kama vile umeme unavyotokea mashariki na kuangaza mpaka magharibi, ndivyo itakavyokuwa kuja kwangu mimi Mwana wa Adamu. 28 Kwa maana po pote ulipo mzoga, ndipo wakusanyikapo tai.

29 “Mara baada ya dhiki ya wakati huo, jua litatiwa giza, mwezi hautatoa mwanga wake tena, na nyota zitaanguka kutoka mbin guni; nguvu za anga zitatikisika. 30 Ndipo itaonekana ishara ya Mwana wa Adamu angani na watu wote ulimwenguni wataomboleza. Nao wataniona mimi Mwana wa Adamu nikija juu ya mawingu ya angani, katika uwezo na utukufu mkuu. 31 Na nitawatuma malaika zangu kwa sauti kuu ya tarumbeta na watawakusanya wateule wangu kutoka pande zote nne za dunia, kutoka mwisho mmoja wa mbingu hadi mwisho mwingine.

32 “Jifunzeni kutoka kwa mti wa mtini. Matawi yake yana poanza kuwa laini na majani kuchipua, mnafahamu kwamba kiangazi kimekaribia. 33 Basi, pia mkiona dalili hizi, fahamuni kwamba amekaribia kurudi, na yu karibu na mlango. 34 Nawaambieni kweli, hakika kizazi hiki hakitapita kabla mambo haya hayajatokea. 35 Mbingu na dunia zitatoweka, lakini maneno yangu hayatapita kamwe.”

Read full chapter