54 Alipo fika mji wa kwao, aliwafundisha watu katika sinagogi lao. Nao wakastaajabu, wakauliza, “Mtu huyu amepata wapi hekima hii na uwezo huu wa kufanya miujiza? 55 Huyu si yule mwana wa seremala? Mama yake si anaitwa Mariamu, na ndugu zake ni Yakobo, Yusufu, Simoni na Yuda? 56 Na dada zake si wako hapa nasi? Amepata wapi basi mambo haya yote?” 57 Wakakataa kumpokea. Lakini Yesu aka waambia, “Nabii hakosi heshima isipokuwa katika nchi yake na nyumbani kwake.”

58 Na hakufanya miujiza mingi huko kwa sababu ya kutokuamini kwao.

Read full chapter