Yesu Anasali Bustanini Gethsemane

32 Wakafika mahali paitwapo Gethsemane, Yesu akawaambia wanafunzi wake, “Kaeni hapa wakati mimi naomba.” 33 Kisha aka wachukua Petro na Yakobo na Yohana. Akawa na huzuni na uchungu mwingi. 34 Akawaambia, “Moyo wangu umejaa huzuni kiasi cha kufa; kaeni hapa mkeshe.” 35 Akaenda mbele kidogo, akajitupa chi ni akaomba kuwa kama ikiwezekana saa hiyo ya mateso aiepuke. 36 Akasema, “Aba, Baba, mambo yote yawezekana kwako. Tafadhali niondolee kikombe hiki cha mateso. Lakini si kama nitakavyo mimi, bali mapenzi yako yatimizwe.” 37 Akarudi, akakuta wame lala. Akamwambia Petro, “Simoni, umelala? Hukuweza kukesha hata kwa saa moja? 38 Kesheni na kuomba msije mkaingia katika majar ibu. Roho i radhi lakini mwili ni dhaifu.” 39 Akaondoka tena akaenda kuomba akisema maneno yale yale. 40 Aliporudi tena ali wakuta wanafunzi wake wamelala; macho yao yalikuwa mazito na hawakujua la kumwambia. 41 Aliporudi mara ya tatu aliwaambia, “ Bado mmelala na kupumzika? Imetosha! Saa imefika. Mimi Mwana wa Adamu ninatiwa mikononi mwa wenye dhambi. 42 Amkeni twendeni, tazameni, yule ambaye amenisaliti amekaribia.”

Read full chapter