Yesu Aingia Yerusalemu

11 Walipokaribia Yerusalemu, wakiwa katika miji ya Bethfage na Bethania katika mlima wa Mizeituni, Yesu aliwatuma wanafunzi wake wawili watangulie. Akawaagiza, “Nendeni kwenye kijiji kile kilichoko mbele yenu. Mtakapokuwa mnaingia kijijini, mtam wona mwana punda amefungwa, ambaye hajawahi kupandwa na mtu ye yote. Mfungueni mumlete hapa. Kama mtu atawauliza, ‘Mbona mnam fungua?’ Mwambieni, ‘Bwana anamhitaji na atamrudisha mara moja.’ ” 4-5 Wakaenda, wakamkuta mwana punda mmoja kando ya barabara, akiwa amefungwa kwenye mlango wa nyumba. Walipokuwa wakimfungua, watu waliokuwa wamesimama karibu wakauliza, “Mbona mnamfungua huyo mwanapunda?” Wakawajibu kama Yesu alivyokuwa amewaagiza, na wale watu wakawaruhusu.

Wakamleta huyo mwana punda kwa Yesu wakamtandikia mavazi yao, akaketi juu yake. 8-10 Watu wengi wakatandaza nguo zao barabarani na wengine wakatandaza matawi waliyokata mashambani. Na wote waliotangulia na wale waliofuata wakapaza sauti zao wakasema: “Hosana! Mungu apewe sifa! Mungu ambariki yeye anayekuja kwa jina la Bwana! Ubarikiwe Ufalme unaokuja wa baba yetu Daudi! Mungu asifiwe!”

11 Yesu akaingia Yerusalemu, akaenda Hekaluni akaangalia kila kitu. Lakini kwa kuwa ilikuwa jioni, akaenda Bethania na wale wanafunzi kumi na wawili.

Read full chapter