11 Wale wakuu wakakasirika sana. Wakaanza kushauriana, “Tumfa nye nini huyu Yesu?’ ’

Kuchaguliwa Kwa Mitume Kumi Na Wawili

12 Siku moja Yesu alikwenda milimani kuomba, akakesha usiku kucha akimwomba Mungu. 13 Asubuhi akawaita wanafunzi wake, na kati yao akachagua kumi na wawili akawapa cheo cha “mitume.” Majina yao ni haya: 14 Simoni, aliyemwita Petro; Andrea, nduguye Simoni; Yakobo; Yohana; Filipo; Bartholomayo; 15 Mathayo; Tomaso; Yakobo, mwana wa Alfayo; Simoni, aliyeitwa Mzalendo; 16 Yuda, mwana wa Yakobo; na Yuda Iskariote, ambaye baadaye alimsaliti Yesu.

Read full chapter