16 Akawaambia wanafunzi wake, “Palikuwa na tajiri mmoja na meneja wake. Ilisemekana kwamba huyo meneja alikuwa anatumia vibaya mali ya tajiri yake. Basi huyo tajiri akamwita meneja wake akamwuliza, ‘Ni mambo gani haya ninayosikia kukuhusu? Nitay arishie hesabu ya mapato na matumizi ya mali yangu kwa maana hutaendelea kuwa meneja tena.’

“Yule meneja akawaza moyoni mwake, ‘Nitafanya nini sasa? Bwana wangu anataka kuniondoa katika kazi yangu. Sina nguvu za kulima, na ninaona aibu kuombaomba! Najua nitakalofanya ili nikipoteza kazi yangu hapa, watu wanikaribishe nyumbani kwao.’

“Kwa hiyo akawaita wadeni wote wa tajiri wake, mmoja mmoja. Akamwuliza wa kwanza, ‘Deni lako kwa bwana wangu ni kiasi gani?’ Akajibu, ‘Galoni mia nane za mafuta ya alizeti.’ Meneja akamwambia, ‘Chukua hati hii ya deni lako, ibadilishe upesi, uan dike mia nne.’ Kisha akamwuliza wa pili, ‘Na wewe deni lako ni kiasi gani?’ Akajibu, ‘Vipimo elfu moja vya ngano.’ Yule meneja akamwambia, ‘ Chukua hati yako, uandike mia nane.’

“Yule tajiri akamsifu yule meneja mjanja kwa jinsi alivy otumia busara. Kwa maana watu wanaojishughulisha na mambo ya dunia hii hutumia busara zaidi kuliko watu wa nuru kukamilisha mambo yao. Nami nawaambieni, tumieni mali ya dunia hii kujipa tia marafiki, ili itakapokwisha mkaribishwe katika makao ya milele.

10 “Mtu ambaye ni mwaminifu katika mambo madogo, atakuwa mwaminifu hata katika mambo makubwa; na mtu ambaye si mwaminifu katika mambo madogo hatakuwa mwaminifu katika mambo makubwa. 11 Na ikiwa hamkuwa waaminifu katika kutunza mali ya dunia hii, ni nani atakayewaamini awakabidhi mali ya kweli? 12 Na kama ham kuwa waaminifu na mali ya mtu mwingine, ni nani atakayewapa mali yenu wenyewe? 13 Hakuna mtumishi awezaye kuwatumikia mabwana wawili. Ama atamchukia mmoja na kumpenda mwingine; au atamheshimu mmoja na kumdharau mwingine. Hamwezi kumtumikia Mungu pamoja na mali.”

Read full chapter