14 Alipokuwa akisema haya akageuka, akamwona Yesu amesimama nyuma yake, lakini hakumtambua! 15 Yesu akamwambia, “Mama, mbona unalia? Unamta futa nani?” Mariamu alidhani aliyekuwa anaongea naye ni mtunza bustani, kwa hiyo akajibu, “Kama ni wewe umemchukua tafadhali nionyeshe ulipomweka ili nimchukue.” 16 Yesu akamwita, “Mar iamu.” Ndipo Mariamu akamgeukia Yesu, akamwambia kwa Kiebrania, “Rabboni!’

Read full chapter