36 Wakati mkiwa na nuru, muitegemee hiyo nuru ili mpate kuwa wana wa nuru.” Baada ya kusema haya, Yesu aliondoka akajificha.

Kutokuamini Kwa Wayahudi

37 Hata baada ya miujiza yote Yesu aliyofanya mbele yao hawakumwamini. 38 Ikawa kama alivyotabiri nabii Isaya aliposema, “Bwana, ni nani ameamini tuliyowaambia? Na ni nani ambaye ameona nguvu za Bwana?” 39 Kwa hiyo hawakuamini, kwa sababu kama Isaya alivyosema tena, 40 “Mungu amewafanya vipofu wasione na mioyo yao ameifanya migumu, ili wasije wakaona kwa macho yao na kuamini kwa mioyo yao, na kumgeukia Mungu awaponye.” 41 Isaya alisema haya kwa kuwa aliona katika maono utukufu wa Yesu na akatabiri juu yake. 42 Hata hivyo wapo wengi, pamoja na viongozi wa Way ahudi, ambao walimwamini, lakini hawakukiri wazi wazi kwa sababu waliwaogopa Mafarisayo, wasije wakafukuzwa kutoka katika masina gogi yao. 43 Wao walithamini zaidi sifa za watu kuliko sifa kutoka kwa Mungu.

Read full chapter