Paulo Amchagua Timotheo

16 Paulo alisafiri mpaka Derbe na Listra ambako mwanafunzi mmoja aitwaye Timotheo aliishi. Mama yake Timotheo alikuwa Myahudi naye alikuwa mwamini; baba yake alikuwa Mgiriki. Timotheo alikuwa mtu mwenye sifa nzuri kwa ndugu wote wa huko Listra na Ikonio. Paulo alitaka amchukue Timotheo awe akisafiri naye, kwa hiyo akamtahiri ili asiwe kikwazo kwa Wayahudi wa eneo hilo ambao walijua ya kuwa baba yake Timotheo alikuwa Mgiriki.

Read full chapter