Unabii Wa Maandiko

12 Kwa hiyo ninakusudia kuwakumbusha hayo siku zote, ingawa mnayafahamu na mmekuwa imara katika kweli mliyo nayo. 13 Nadhani ni vema niwahimize kwa kuwakumbusha mambo haya, wakati wote nina poishi katika mwili huu. 14 Kwa maana najua kwamba karibu nitauweka kando mwili wangu, kama Bwana wetu Yesu Kristo alivyon ionyesha wazi. 15 Na nitahakikisha kwamba baada ya kuondoka kwangu mtaendelea kukumbuka mambo haya kila wakati.

16 Tulipowafundisha juu ya uweza na kuja kwa Bwana wetu Yesu Kristo, hatukufuata hadithi zilizotungwa kwa werevu, bali tulish uhudia kwa macho yetu utukufu wake. 17 Maana alipopewa heshima na utukufu kutoka kwa Mungu Baba, na sauti ikamjia katika utukufu mkuu ikisema, “Huyu ni Mwanangu mpendwa, nimependezwa naye’ 18 tuliisikia sauti hii iliyotoka mbinguni, maana tulikuwa naye kwenye ule mlima mtakatifu.

19 Kwa hiyo tuna uhakika zaidi juu ya ujumbe wa manabii. Hivyo itakuwa vema mkizingatia ujumbe huo, kama vile watu wanavy oitegemea taa ing’aayo mahali penye giza, mpaka Siku ile itakapo fika na nyota ya asubuhi itakapoangaza mioyoni mwenu. 20 Kwanza kabisa ni lazima muelewe kwamba hakuna unabii katika Maandiko uliotokana na tafsiri ya nabii mwenyewe. 21 Kwa sababu hakuna unabii uliokuja kwa matakwa ya binadamu, bali watu walinena ujumbe kutoka kwa Mungu wakiongozwa na Roho Mtakatifu.

Read full chapter