Msiny imane, isipokuwa kama mmekubaliana kufanya hivyo kwa muda mfupi ili muwe na nafasi nzuri ya maombi. Lakini baada ya muda huo rudianeni tena shetani asije akapata nafasi ya kuwajaribu kwa sababu ya kushindwa kujizuia. Nasema haya kama ushauri, na si sheria. Ningalipenda wote wawe kama mimi nilivyo. Lakini kila mtu amepewa karama yake kutoka kwa Mungu, mmoja ana karama hii na mwingine ana karama ile.

Na sasa nasema kwa wale wasioolewa na kwa wajane. Ingekuwa vizuri kama wangeendelea kuishi bila kuoa au kuolewa kama mimi.

Read full chapter