Kwa maana niliyopokea ndio niliyowapa ninyi, nayo ni muhimu sana: kwamba Kristo alikufa kwa ajili ya dhambi zetu, kama ilivy oandikwa katika Maandiko. Na kwamba alizikwa na kufufuka siku ya tatu, kama ilivyoandikwa katika Maandiko. Na kwamba alimto kea Kefa, kisha akawatokea wale kumi na wawili. Baadaye akawa tokea ndugu waamini zaidi ya mia tano kwa pamoja, na wengi wao wangali hai, ingawa wengine wameshakufa. Kisha akamtokea Yakobo, na ndipo akawatokea mitume wote. Na mwisho wa wote, akanitokea na mimi, ambaye ni kama nilizaliwa kwa hali isiyo ya kawaida.

Read full chapter