Chakula Kilichotolewa Sadaka Kwa Sanamu

Sasa kuhusu chakula kilichotolewa sadaka kwa sanamu. Tuna jua kwamba ‘sisi sote tuna ujuzi.’ Lakini ‘ujuzi’ huleta maji vuno, ila upendo hujenga. Mtu anayedhania kwamba anajua kitu, basi hajafahamu kama inavyompasa kujua. Lakini kama mtu anam penda Mungu, mtu huyo anajulikana na Mungu.

Kwa hiyo basi, kuhusu kula chakula kilichotolewa sadaka kwa sanamu: tunajua kwamba ‘sanamu haina uhai wa kweli’ na kwamba ‘kuna Mungu mmoja tu.’ Kwa maana hata kama wapo hao wanaoitwa ‘miungu,’ kama ni mbinguni au duniani; na kwa kweli wapo ‘miungu’ wengi na ‘mabwana’ wengi; sisi tunajua kwamba kuna Mungu mmoja, aliye Baba, ambaye vitu vyote vinatoka kwake, na sisi tunaishi kwa ajili yake; na kuna Bwana mmoja, Yesu Kristo, ambaye vitu vyote vimekuwepo kupitia kwake na tunaishi kutokana naye.

Lakini si wote wanajua mambo haya. Watu wengine mpaka leo bado wamezoea miungu ya sanamu kiasi ambacho wanapokula chakula hicho wanadhani ni chakula kilichotolewa kwa sanamu, na kwa kuwa dhamiri yao ni dhaifu, inadhurika. Lakini chakula hakitusaidii kuwa karibu zaidi na Mungu. Hatupotezi cho chote tusipokula, wala hatupati faida yo yote kama tukila.

Lakini hata hivyo tuwe waangalifu jinsi tunavyotumia uhuru wetu tusije tukawakwaza walio dhaifu katika imani. 10 Kwa maana kama mtu mwenye dhamiri dhaifu akiwaona ninyi wenye ujuzi mkila katika hekalu la sanamu, je, si atavutwa kula chakula kilichoto lewa kwa sanamu? 11 Kwa njia hiyo, huyo ndugu mwenye dhamiri dhaifu, ambaye Kristo alimfia, atateketea kwa sababu ya ujuzi wako. 12 Mnapowatenda dhambi ndugu zenu kwa njia hii na kuharibu dhamiri zao dhaifu, mnamkosea Kristo. 13 Kwa hiyo kama chakula kitamfanya ndugu yangu aanguke katika dhambi, sitakula nyama kamwe, nisije nikamfanya ndugu yangu aanguke.