Kutoka kwa Paulo, mtume wa Kristo Yesu kwa amri ya Mungu Mwokozi wetu na ya Kristo Yesu aliye tumaini letu. Kwa

Walimu Wa Uongo

Kama nilivyokusihi wakati nikienda Makedonia, napenda ukae hapo Efeso uwaamuru watu fulani wasiendelee kufundisha mafund isho ya uongo. Pia wasiendelee kupoteza wakati wao kwa hadithi na orodha ndefu zisizo na mwisho za majina ya vizazi ambazo huchochea mabishano badala ya kuwajenga katika maarifa ya kimungu yatokanayo na imani. Shabaha ya maagizo haya ni upendo utokao katika moyo safi, dhamiri njema na imani ya kweli. Watu wengine wamepotoka na kuingia katika majadiliano yasiyo na maana kwa kuwa hawakuzingatia mambo haya. Wanataka kuwa walimu wa sheria ingawa hawaelewi mambo wanayosema wala hayo wanayotilia mkazo.

Tunajua kwamba sheria ni njema iwapo inatumika ipasavyo. Lakini tuelewe kwamba sheria haikuwekwa kwa ajili ya wenye haki, bali kwa ajili ya waasi na wasiotii: wasiomcha Mungu na wenye dhambi; wale wasio watakatifu, walio wachafu; wale wanaow aua baba zao na mama zao; wale wanaoua binadamu; 10 wale wal iowazinzi, wafiraji; wale wanaoteka watu nyara, na waongo, na wanaoapa kwa uwongo; na mengine mengi ambayo ni kinyume cha mafundisho ya kweli, 11 ambayo yanaambatana na Injili tukufu ya Mungu Mbarikiwa, ambayo nimekabidhiwa. 12 Nami namshukuru Kristo Yesu Bwana wetu, aliyenitia nguvu na kunihesabu kuwa ni mwaminifu kwa kunichagua nimtumikie. 13 Ingawa hapo mwanzo nilimkufuru na kumtesa na kumtukana, nili hurumiwa kwa sababu nilitenda hayo katika ujinga wangu na kutoku amini kwangu. 14 Na neema ya Bwana wetu ilimiminika tele kwa ajili yangu pamoja na imani na upendo uliomo ndani ya Kristo Yesu. 15 Neno hili ni la hakika tena linastahili kukubalika kabisa, kwamba Kristo Yesu alikuja duniani kuokoa wenye dhambi, ambao kati yao, mimi ni mwenye dhambi kuliko wote. 16 Lakini nilihurumiwa kwa sababu hii kwamba, kwa kunitumia mimi niliyekuwa mwenye dhambi kuliko wote, Kristo aonyeshe uvumilivu wake, niwe mfano kwa wote watakaomwamini na kupata uzima wa milele. 17 Basi, heshima na utukufu ni wake yeye Mfalme wa milele, asi yekufa wala asiyeonekana, aliye peke yake Mungu, milele na milele. Amina.

18 Mwanangu Timotheo, ninakukabidhi agizo hili, kufuatana na maneno ya unabii yaliyosemwa juu yako, ili kwa kuyafuata uweze kupigana ile vita njema, 19 ukishikilia imani na dhamiri njema. Watu wengine, kwa kukataa kuisikiliza dhamiri yao, wameangamiza imani yao. 20 Miongoni mwa watu hao wamo Himenayo na Aleksanda ambao nimewakabidhi kwa shetani, ili wajifunze wasimtukane Mungu.